Utangulizi

Shughuli za Uwekezaji katika Mfuko zinafanywa kwa mujibu wa Sera ya uwekezaji na miongozo mbalimbali ikiwemo ile ya BOT na SSRA. Miongozo hiyo huelekeza maeneo ya uwekezaji, viwango vya riba na kiasi cha kuwekeza kwa kuzingatia mpango wa uwekezaji kwa mwaka husika. Uwekezaji huzingatia dhima na madeni mengine ya kifedha yanayotarajiwa kuukabili Mfuko kwa kipindi husika.

Madhumuni ya shughuli za Uwekezaji

 • Lengo kuu la kuwekeza fedha zinazokusanywa ni kuujengea Mfuko uwezo wa kutoa mafao na huduma bora kwa wanachama na wateja.
 •  Uwekezaji hufanyika kwa umakini mkubwa iIi kupata faida, kulinda thamani ya mtaji, kuhakikisha wakati wote Mfuko una fedha za kutosha kulipia mafao ya wanachama kulingana na stahili zao na kwa kuzingatia misingi bora ya uwekezaji inayokubalika kitaifa na kimataifa.

Misingi ya Uwekezaji

 •  Usalama - Kuwekeza kwenye maeneo ambayo ni salama iIi fedha za wanachama zisipotee (Safety)
 • Faida - Kuwekeza kwenye vitegauchumi vyenye kuleta mapato makubwa (Yield)
 • Ukwasi - Kuwekeza kwa utaratibu ambao wakati wote Mfuko utakuwa na fedha za kutosha kulipia mafao na matumizi mengine (Liquidity)
 • Manufaa kwa jamii "Socio Economic Utility"- kuwekeza katika maeneo ambayo yatakuwa na manufaa makubwa kiuchumi na kijamii.

Maeneo ya Uwekezaji

 •  Yafuatayo ni maeneo ambayo LAPF huwekeza rasilimali zake.
 • Dhamana za Serikali (Treasury bonds, Treasury Bills & stocks);
 • Hati Fungani za Makampuni (Corporate bonds);
 • Amana za Mabenki (Fixed deposits);
 • Hisa za Makampuni (Equities);
 •  Mikopo (Loans); 
 • Miradi ya Majengo (Real Estates)