Pensheni ya Uzee

LAPF hutoa mafao ya pensheni ya uzee ambayo hulipwa kwa mwanachama ambaye: -

  • Ametimiza umri wa kustaafu miaka 55 na kuendelea hadi miaka 60 kwa lazima;
  • Amechangia katika Mfuko kwa muda usiopungua miaka 15 au miezi 180

Kiwango cha pensheni atakacholipwa mstaafu kinategemea mshahara wake wa wakati anastaafu na muda aliochangia katika mfuko wakati wa utumishi wake. Kumbukumbu zinazohitajika zimeorodheshwa katika fomu ya maombi ya mafao hayo ijulikanayo kama LAPF/BEN.l

Pensheni ya Uzee inalipwa kwa makundi mawili

  • Malipo ya Mkupuo
  • Malipo ya kila Mwezi

Ukokotoaji wa Pensheni

Pensheni ya uzee inapatikana kwa kanuni ifuatayo

Pensheni = 1/540 X (miezi ya uchangiaji)  (mshahara juu kabisa ndani ya miezi 12 kabla ya tarehe ya kustaafu x 12)

  • Malipo ya kila mwezi= (Pensheni / 2) X 1/12
  • Malipo ya mkupuo=1/2  X  (Pensheni)  X 15.5

Muhimu: Mwombaji anaweza kuamua kuchukua kiwango chochote cha malipo ya mkupuo alimradi hakitazidi asilimia 50 au nusu ya pensheni.

Endapo mwanachama aliyestaafu hakuwa amechangia LAPF kwa miaka 15 basi atalipwa tu kiinua mgongo ambacho ni sawa na pensheni x 5. Malipo haya hulipwa mara moja tu.