Pensheni ya Urithi

Endapo mwanachama atafariki dunia akiwa katika utumishi na akiwa amechangia LAPF kwa muda wa miaka 15, wategemezi wake watalipwa pensheni ya urithi. Wategemezi hao ni pamoja na mjane/mgane, watoto au wazazi. Kanuni ya kukokotoa mafao ya warithi ni sawa na ile ya mafao ya uzee.

Mafao haya hulipwa moja kwa moja kwa wategemezi au kupitia kwa msimamizi aliyeteuliwa na wanandugu na kuthibitishwa na mahakama. Pensheni kwa watoto hulipwa hadi wanapofikia umri wa miaka 21 au 25 kwa mtoto mlemavu.

 

Ukokotoaji wa Pensheni

Pensheni ya uzee inapatikana kwa kanuni ifuatayo

Pensheni = 1/540 X (miezi ya uchangiaji)  (mshahara juu kabisa ndani ya miezi 12 kabla ya tarehe ya kustaafu x 12)

  • Malipo ya kila mwezi= (Pensheni / 2) X 1/12
  • Malipo ya mkupuo=1/2  X  (Pensheni)  X 15.5