Pensheni ya Ulemavu

Pensheni ya ulemavu inalipwa kwa mwanachama aliyepata ulemavu wa kimwili na kiakili akiwa kazini, kiasi cha kukosa uwezo wa kue delea nakazi na kujipatia kipato.

Sifa za Mwombaji 

  • Mwombaji awe amepata ulemavu wa kudumu
  • Awe amepoteza kabisa uwezo wa kufanya kazi na kujipatia kipato
  • Awe amechangia kwa miaka 15 iIi kupata pensheni

Mafao yanayotolewa

Pensheni atakayolipwa ni pensheni ya kawaida ya kustaafu ikiwa ni malipo ya mkupuo na pensheni ya kila mwezi tangu pale alipopata ulemavu kulingana na muda aliochangia kwenye Mfuko hadi hapo atakapofariki dunia.