Msaada wa mazishi

Mafao haya hulipwa kwa wafiwa kusaidia sehemu ya gharama za mazishi ya mwanachama wa LAPF. Katika mpango huu yeyote ambaye ameteuliwa kusimamia shughuli za mazishi anaweza kuomba msaada huo wa mazishi. Msaada huo hutolewa endapo marehemu alichangia kwenye mfuko kwa angalau miezi sita kabla ya kifo chake. Msaada unaotolewa ni fedha taslimu kiasi cha ni Sh. 250,000/-  ambazo huingizwa moja kwa moja kwenye akaunti ya benki ya msimamizi wa mazishi (mwombaji). Msaada huu haupunguzi kwenye mafao ya mirathi. ;