Michango

Mifumo mingi ya hifadhi ya jamii duniani inaendeshwa kwa wanachama kuchangia kiasi kilichokubalika. Sheria ya LAPF Na. 9 ya mwaka 2006 inawataka waajiri na wanachama kujiandikisha na kuwasilisha michango yao kwa wakati uliowekwa. Uchangiaji katika Mfuko umewekwa kwa viwango mbalimbali kulingana na aina ya uanachama.

Michango ya Lazima

Kwa mujibu wa Sheria ya LAPF Na. 9 ya mwaka 2006, kifungu cha 19, mwanachama anayechangia kwa mujibu wa Sheria anatakiwa kuchangia kiasi cha asilimia tano (5%) na mwajiri anamchangia nyongeza ya asilimia kumi na tano (15%) ya mshahara wake. Kwa mwanachama aliye katika ajira ya sekta binafsi huchangia asilimia kumi (10%) na waajiri asilimia kumi (10%) ya mshahara wa mwanachama na hivyo kufanya michango yote kuwa asilimia ishirini (20%).

Michango ya Hiari

Kifungu cha 17 (1) & (2) cha Sheria ya LAPF kinatoa uhuru kwa mwanachama wa hiari kuamua kiwango anachotaka kwa muda atakaoamua ilimradi jumla yake kwa mwezi isiwe chini ya Sh. 20,000/=.

Uwasilishaji Michango

Katika Sheria ya LAPF kifungu cha 19(2) kinamtaka mwajiri kuwasilisha michango ya lazima ya mwanachama aliyeandikishwa LAPF ndani ya siku 30 baada ya mwezi unaohusu makato hayo kupita. Njia mbalimbali za uwasilishaji michango ya wanachama zinakubalika kama vile:-

 • Kupokea moja kwa moja kutoka Hazina,
 • Kutumia huduma za kibenki (telegraphic transfers, Bank deposits) au TISS
 • Kutuma hundi kupitia rejista ya posta, EMS au DHL n.k.
 • Kuwatuma watumishi wa ofisi husika kuwasilisha hundi kwenye ofisi za LAPF.
 • Wakaguzi wa LAPF kuchukua hundi za michango wanapotembelea waajili.
 • Kutumia utaratibu wa utumaji wa fedha kupita mitandao ya simu (airtelmoney) kwa wachangiaji wa hiari waliojiajiri.
 • Kutoa maelekezo benki (standing order) kuwa kiasi fulani kitolewe kwenye akaunti na kuingizwa kwenye akaunti ya LAPF kila mwezi au kwa muda ulioamuliwa kwa wachangiaji wa hiari.

Mambo Muhimu katika Uwasilishaji

 • Michango Michango ya wanachama wa lazima lazima iwe kamili yaani asilimia ishirini (20%)
 • Orodha ya wanaochangia lazima iambatanishwe na Hundi kwa wale wanaotuma hundi kwa posta (kutumia fomu maalumu ya LAPF/CON.I).  Kwa malipo yanayopita benki moja kwa moja orodha watumishi wanaolipiwa inapaswa kuwasilishwa mara baaoa ya malipo kufanyika.
 • Kama fedha zimetumwa kwa kutumia benki ni y,yema nakala ya risiti ya kutuma fedha hizo (TT Receipt) ikaambatanishwa na kumbukumbu za makato deductions sheets zikatumwa kwenye ofisi ya LAPF kwa urahisi wareJea.
 • Kiasi cha michango ya wanachama ni lazima kilingane na jumla ya fedha zilizoandikwa kwenye hundi.

Jukumu la LAPF katika kuhakikisha Michango inawasilishwa

IIi kuhakikisha Waajiri na Wanachama wanatekeleza jukumu lao la kuwasilisha michango, Mfuko hutumia Wakaguzi wake ambao hufanya kaguzi mara kwa mara kwa lengo la

a) kuhakiki uandikishaji na ukamilifu wa kumbukumbu za wanachama;

b) kuhakiki michango inawasilishwa kwa wakati na kwa kiwango kinachotakiwa;

c) maandalizi ya mafao yanafanywa mapema kabla ya muda wa kustaafu;

d) Kujibu hoja mbalimbali zinazojitokeza kwa waajiri au wanachama.