Mafao ya uzazi

Mafao ya uzazi ya LAPF hulipwa kwa wanachama wanawake waliojifungua watoto.

Sifa za Mwombaji 

  • Awe amechangia kwenye Mfuko kwa kipindi kisichopungua miaka miwili
  • Awe amefikia kipindi cha kujifungua na amejifungua mtoto.
  • Hulipwa kila baada ya miaka mitatu isipokua pale ambapo mtoto amefariki wakati alipozaliwa au kabla ya kupita miaka hiyo mitatu.
  • Madai yanapaswa kuwasilishwa ndani ya siku 90 baada ya kujifungua

Mafao yanayotolewa

Mafao haya ni fedha taslimu kiasi cha asilimia arobaini ya mshahara wa wiki kumi na nne wa mwanachama sawa na asilimia 129.3% ya mshahara wa mwezi alipojifungua.