Huduma nyingine

Pamoja na mafao hayo LAPF inatoa pia huduma nyingine kama vile kumuandaa mwanachama kustaafu. Huduma hizo zinamuwezesha mwanachama kujijengea nyumba na au kuwa na mradi wa kumpatia kipato. Huduma hizo ni: -

Mikopo ya Nyumba

LAPF inatoa mikopo ya nyumba kwa wanachama wake wanaokaribia kustaafuu kwa lengo la kuwasaidia mahitaji ya nyumba kabla ya kustaafu. Riba inayotozwa katika mikopo hiyo ni 7% tu.

Sifa za Mwombaji

IIi kupata mkopo huo mwanachama anatakiwa: -

  • Kuwa amechangia kwa kipindi kisichopungua miezi 180 au miaka 15
  • Kufikisha umri wa miaka 55 na kuendelea. Mkopo unaotolewa hauzidi nusu ya malipo ya mkupuo ambayo angepata endapo angekuwa amestaafu kawaida.

Mfano

  • Pensheni ya Uzee
  • Umri = miaka 55 hadi 59
  • Miaka isiyopungua 15 ya kuchangia LAPF
  • Pensheni = 1/540 x (miezi ya uchangiaji) x (mshahara wa alioombea mkopo x 12).
  • Malipo ya mkopo si zaidi ya =(1/2 x (Pensheni) x 15.5)/2

Mikopo ya Wanachama kupitia SACCOS

Katika kuboresha maisha ya Wanachama, LAPF ina makubaliano na Vyama vya Kuweka na Kukopa (SACCOS) zenye wanachama wachangiaji ya kutoa mikopo yenye 1engo 1a kuwawezesha kujihusisha na shughuli za kujipatia kipato cha ziada. Katika utaratibu huu LAPF hutoa kiasi cha fedha kwa SACCOS kama walivyoomba kulingana na sifa zilizowekwa na hatimaye SACCOS hizo kutoa mikopo kwa wanachama. LAPF imeweka riba ya chini sana katika fursa hii kama sehemu ya kuwanufaisha wanachama wake.

Vigezo vya kupata Mkopo

  • Barua ya udhamini kutoka kwa Mwajiri
  • Taarifa ya hesabu zilizokaguliwa za miaka mitatu.
  • Taarifa ya benki (Bank Statement) inayoonyesha historia ya u1ipaji wa mikopo pamoja na mali ya SACCOS isiyohamishika.